Abbah atia neno sakata la Marioo na Mbosso

Abbah atia neno sakata la Marioo na Mbosso

Ooooooh!!! Kivumbi leo, bwana bwana kumekuwa na sintofahamu kati ya wanamuziki wa kizazi kipya Mbosso Khan na Marioo baada ya mzee wa amepotea kutoalikwa katika show ya Marioo, kumezua mambo mengi ambayo tulikuwa hatuyajui, waswahili wanakamsemo kao kuwa safari moja huanzisha nyingine ndicho kilichotokea kwa wamba hawa wawili.

Ukiendelea kusoma utaelewa nini nazungumzia kuhusiana na msemo huo hapo juu, unaambiwa siku hizi bwana wachawi sio wazee, ukiachilia na maneno yanayozuka mitandaoni kumbe wana wanamadukuduku yako moyon.

Mmoja ya chombo cha habari kilifanya mahojiano na Mbosso ameonekana kuumizwa na kushangazwa na Marioo jinsi anavyomchukulia mpaka kutomwalika katika show yake ambayo bosi wake wa wasafi, Diamond alialikwa.

Kwa mujibu wa Kirungi ameeleza kuwa, akitoa nyimbo naye Marioo anatoa kama kuna bifu la chini chini kati ya mtu moja au wote wawili hawataki kuweka wazi mafansi wao wajue nini kinaendelea.

Team Scoop haina desturi ya kuacha mambo yenye ukakasi kama hayo moja kwa moja tukamvutia waya Abbah ambaye ni meneja wa Marioo yeye ana ilichukuliaje hilo suala.

“Kuna vitu vyengine inabidi wao wenyewe kama wasanii waitane wazungumze wajue wapi kunashida kwa sababu wao ni washkaji yawezekana Marioo kumwambia Mbosso amempandishia nyimbo labda ilikuwa ni utani ukizingatia ni marafiki hawajawahi kugombana,” alisema Abbah.

Huku swala la Marioo kutomualika Mbosso katika show yake alifunguka na kueleza kuwa ni maamuzi ya mtu binafsi aliyeandaa show yake.

Kwa upande wa Bad (Marioo) hakulikalia kimya swala hili akaona isiwe tabu afunike kombe mwanaharamu apite na kuamua kumuomba msamaha mwanamuziki mwenzake.

“Mimi namheshimu kila mtu katika kazi na kuhusu kumpandishia nyimbo kila mtu anahitaji kuwa juu ya mwenzake, sasa nikiona mtu anatoa kazi nzuri lazima niweke ushindani na mimi nifanye zaidi” amesema Marioo

Japo kinyonge mwamba huyo alimtaka radhi msanii mwenzake kwa kusema “hatuna sababu ya kugombana sisi sote ni wanadamu tuna muomba Mungu, tusimkaribishe shetani tusameheane tuchape kazi no hard fellings”alisema Marioo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags