A$ap alivyo pafomu kwenye ndege

A$ap alivyo pafomu kwenye ndege


Rapa na mkali wa mitindo tokea Marekani, A$ap Rocky ameingia kwenye vichwa vya habari baada ya kutumbuiza akiwa kwenye ndani ya 'Helicopter' kwenye tamasha la muziki la Rolling Loud.

A$ap alikuwa msanii kinara kwenye tamasha hilo lililofanyika usiku wa kuamkia leo katika viwanja vya Hollywood Park Ground, California.

Tamasha hilo ambalo pia lilitoa nafasi kwa wasanii wengine kutumbuiza kama YG, Sexy Red, Ski Maski na wengine wengi linaendelea leo huku msanii kinara akiwa Play Boy Carti akiwana na wengine ni Kern Carson, Blxst, Quavo, Greedo na wengine weingi.

Carti ambaye ni kinara leo Machi 16, 2025 kwenye tamasha hilo anatarajiwa kufanya makubwa kwani Ijumaa ya Machi 14 aliachia album yake ya tatu ya studio aliyoipachika jina la 'I Am Music'.

Ambapo amewashirikisha wasanii kama Kendrick ambaye ametokea kwenye nyimbo tatu “Mojo Jojo,” “Backd00r,” na “Good Credit. Lakini pia wasanii wengine walioshirikishwa kwenye album hiyo ni pamoja na Travis Scott, the Weeknd, Skepta, Future, Lil Uzi Vert, Ty Dolla Sign and Young Thug.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags