Remix zinavyo nogesha nyimbo

Remix zinavyo nogesha nyimbo

Wasanii wa muziki wamekuwa na utaratibu wa kuzirudia nyimbo zao ambazo tayari zimetolewa na kuzifanya kwa mtindo mwingine'Remix'.

Kawaida remix hizo huhusisha zaidi kubadilisha verse zao kwa kuimba mada tofauti na ile waliyoimba mwanzo au kumshirikisha msanii ambaye atatia verse mpya kwenye wimbo huo. Na muda mwingine hubadilisha mirindimo na namna ya mapigo kwenye biti za nyimbo hizo au vyote kwa pamoja.

Mfano wimbo wa Tunashine wa kwake P-Funk Majani ft Conboi Cannabino X Rapcha ambao biti lake limebadilishwa kutoka kwenye wimbo wa 'Kimya Kimya' wa kwao Jay Moe ft Ngwea ambao pia ulitayarishwa na Producer P-Funk Majani.

Zipo remix nyingi kwenye historia ya muziki wa Bongofleva ambazo zimefanya vizuri na kuwaletea matunda wasanii waliyoshiriki kwenye nyimbo hizo.

Zigo remix, hii ni ile ya wimbo wa 'Zigo' wa kwake Masta AY ambayo ilimkutanisha na Diamond Platnumz ilitoka Januari 22, 2016. ikiwa kama moja ya Remix classic ilifanikiwa kuleta mapinduzi makubwa ya wimbo huo. Video yake ikifanikiwa kutazamwa mara milioni 24,584,217 pale YouTube ukiwa ndio wimbo pekee uliyotazamwa mara nyingi zaidi.

Songi Songi Remix, ngoma ya mwanadada kutokea DRC Congo, Maud Elka aliyemuweka King Kiba kwenye remix hiyo ambayo iliachiwa Agasti 20, 2021. Awali wimbo Original uliachiwa Machi, 2021 ukiwakutanisha Maud Elka na Hiro.

Fresh Remix, ngoma ya kwake Farid Qubanda 'Fid Q' aliyomshirikisha Diamond Platnumz na Rayvanny ambaye aliingia kwa kujipenyeza kwenye Remix hiyo kwa mujibu wa maelezo ya Fid Q . Fresh remix iliachiwa Agasti 21, 2017 lakini Original ya wimbo huo ulitoka Agasti 13, 2017 ambayo ni siku ya kumbukizi ya kuzaliwa rapa huyo kutokea Mwanza ambaYe amekuwa akiachia zawadi ya wimbo kwa mashabiki zake kila ifikapo siku hiyo.

Remix ya wimbo huo kwa mara nyingine tena ilionesha uwezo wa kurap kwa msanii Diamond Platnumz ambaye kabla ya kufanya vizuri kwenye muziki wa kuimba Bongofleva na R&B alikuwa rapa.

My Boo remix, Audio ya wimbo huo iliachiwa Julai 22, 2019 ikiwa kama remix ya kwao Harmonize X Q Chief. Hapo awali wimbo huo uliachiwa miaka ya nyuma. Remix ya wimbo huo imetazamwa zaidi ya mara milioni 19 kwenye mtandao wa Youtube.

Distance Remix, Ngoma ya kwake Jay Rox kutokea Zambia aliyowashirikisha Rayvanny na AY. Remix hiyo ilitoka mwaka 2019, Origina ya wimbo huo wa Distance ya Jay Rox aliwashirikisha The Kansoul kutokea Kenya.

Remix ya wimbo huo ilifanikiwa kufanya vizuri kwenye mipaka ya Afrika Mashariki huku video yake ikiwa imetazamwa zaidi ya mara milioni 2 Youtube.

My Number One Remix, Miongoni mwa remix kali ambazo zinahistoria kubwa kwenye muziki wa Bongofleva ni baada ya kuwakutanisha staa wa Bongofleva Diamond Platnumz na Davido kutokea Nigeria. Huku video ya ngoma hiyo mpaka sasa ikiwa imetazamwa zaidi ya mara milion 55.

Original ya wimbo huo ilitoka 2013 Diamond akiimba mwenyewe huku remix ya wimbo huo ikitoka 2014 Januari.

Yule Remix, ngoma ya kwake AY aliyomshirikisha Marioo iliachiwa Juni 7, 2024 na video yake imefanikiwa kutazamwa zaidi ya mara milioni 1 kwenye mtandao wa youtube. Hii ni heshima kubwa kwa Marioo kuipata remix ya wimbo mkubwa wa Yule kutoka kwa nguli mkubwa wa Bongo fleva AY.

Bed Room Remix, Ngoma ya kwake Harmonize aliyowashirikisha rappers tofauti tofauti kutokea kwenye kiwanda cha muziki Tanzania ambao ni Darassa, Country Boy, Young Lunya, Moni, Billnas, Rosa Ree, na Baghdad. Bed Room remix iliachiwa 2020.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags