8 wauawa Syria

8 wauawa Syria

Zaidi ya watu 8 wauwawa wakiwemo watoto watatu kwa mabomu yaliyokuwa ndani ya gari katika matukio mawili tofauti kaskazini mwa nchi ya Syria siku ya jumapili.

Shirika linalofuatilia masuala ya vita limesema mlipuko mmoja ulipiga katika duka la kutengeneza magari huko Shawa, kijiji kilicho karibu na mpaka wa nchi ya Uturuki unaoshikiliwa na wapiganaji wanaoiunga Ankara.

Aidha baadha ya raia waliambia moja ya chombo cha habari kuwa watu watano wakiwemo watoto watatu waliuawa na wengine 10 kujeruhiwa.

Shirika linalofuatilia haki za binadamu nchini humo lenye makao yake nchini Uingereza limesema maeneo yanayoshikiliwa na Uturuki pamoja na washirika wake wa Syria huko kaskazini mwa nchi hiyo panapotokea mauaji ya mara kwa mara.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags