5 wafariki kwa ugonjwa usiojulikana Kagera

5 wafariki kwa ugonjwa usiojulikana Kagera

Serikali kupitia Wizara ya Afya imetoa tahadhari juu ya uwepo wa ugonjwa ambao bado haujajulikana mkoani Kagera, katika Wilaya ya Bukoba Vijijini, ambapo watu 7 wanasadikika kupata dalili za homa, kutapika, kutokwa damu maeneo mbalimbali ya mwili na figo kushindwa kufanya kazi. Hadi sasa watu watano kati yao wamefariki na wengine wawili wako hospitalini wakiendelea na matibabu.

Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Tumaini Nagu ametoa taarifa hiyo jana katika ofisi za Wizara, Jijini Dodoma.

“Wizara imepokea taarifa za uwepo wa ugonjwa ambao bado haujajulikana Kagera, Bukoba Vijijini, Kata ya Maruku na Kanyangercko, Vijiji vya Bulinda na Butayaibega, mwenendo wa ugonjwa huu unaashiria uwezekano kuwa ni ugonjwa wa kuambukiza, hivyo Serikali inaendelea kufuatilia kwa karibu kuhusu mwenendo wa ugonjwa na kuchukua hatua za kudhibiti ili usisambae,” amesema Prof. Tumaini.

Aidha, amewataka wananchi kuwahi kituo cha kutolea huduma za afya kwa ajili ya uchunguzi na matibabu endapo ataona dalili kama kupatwa na homa, kutapika, kuharisha, kutoka damu na mwili kuishiwa nguvu,

Pia amewakumbusha kuwahi kutoa taarifa mapema kwenye kituo cha kutolea huduma kilicho karibu au kupiga simu namba 199 bila malipo endapo utamuona au kukutana na mtu mwenye dalili kama hizo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post