Watu 39 wamefariki katika ajali ya moto, katika kituo cha wahamiaji nchini Mexico. Tukio hilo limetokea katika mji wa Ciudad Juarez, ambapo idadi ya waliojeruhiwa ni 29, huku maafisa wakidai moto umetokea wakati wahamiaji 68 waliokuwa kituoni hapo wakipinga kufukuzwa.
Asilimia kubwa ya waathirika wametokea Amerika ya Kati na Kusini katika Nchi za Guatemala, Honduras, Elsavador, Venezuela, Colombia na Ecuador wakiwa na lengo la kwenda Marekani.
Aidha, Rais wa Mexico, Andres Manuel Lopez Obrador alieleza kuwa wahamiaji hao waliposikia watarudishwa katika nchi zao wakachoma moto kituo kupinga uamuzi huo.
Leave a Reply