Mkuu wa utumishi wa umma kutoka nchini Kenya Felix Koskei ametoa uamuzi wa kuwasimamisha maafisa 27 kwa kuingiza sokoni sukari ilio haribika dhidi ya mdhibiti mkuu wa viwango.
Taarifa imeeleza mifuko 20,000 ya sukari iliingizwa nchini humo mwaka 2018 na kuzuiwa na mdhibiti wa viwango baada ya kubainika haifai kwa matumizi ya binadamu na ilihifadhiwa kwaajili ya kubadilishwa kuwa kemikali ya 'ethanol'.
Kwa mujibu wa Koskei, uchunguzi umebaini maafisa hao walipuuza majukumu yao bila kujali athari itakayotokea kwa umma wakati ambapo wananchi wanakabiliwa na ongezeko kubwa la bei ya sukari kutokana na uhaba.
Leave a Reply