“Harmonize akiziona picha za Kajala ataweka bango stend ya Magufuli”

“Harmonize akiziona picha za Kajala ataweka bango stend ya Magufuli”

Wakati Kajala akiendelea na heka heka za maandalizi ya birthday yake, anayotarajia kusherekea tarehe 22 mwezi huu, mashabiki nao hawajakaa mbali wameendelea kutupia comment za uchokozi kwa ‘staa’ huyo wa filamu nchini.

Kupitia picha mpya za nyota huyo, maneno ya kichokozi kutoka kwa mashabiki yametawala wengi wao wamekuwa wakihusianisha picha hizo na jina la @harmonize_tz, huku wengine wakikosea mavazi ya bibie huyo aliyovaa katika picha hizo.

Kupitia comment za mashabiki kuhusu #Harmonize, zinaonesha  huenda watu wengi bado wanatamani penzi la wawili hao lingeendelea kuwepo hadi leo.

Kati ya Comment za mashabiki zinasema,

“Mamaaaa!!! HARMONIZE Akiziona Hizi Picha Lazima Aweke Bango Lingine Pale Stend ya Magufuli Mbezi...😥🙌🚶‍”, ameandika @timothy_malyii

“@kajalafrida ifike mahali ubadilike wewe ni mama hayo mambo sio ya kufanya huku, tunajua wewe ni mzuri wa sura na umbo haina haja ya kukaa mikao ya kujiachia ovyo na kuvaa nguo za wazi kuonyesha maumbile yako shepu unayo na sura unayo nguo yoyote ukivaa unapendeza hasa za kujisitiri jiamini dada yangu, unafanya na kukaa kama sio mama sijui unatafuta nini dada angu embu badilika najua hayanihusu ila nimejisikia tu kukupa ushauri kama mdogo wako ukitaka chukua ukitaka achana nao halafu pita kushoto,pole sana hope Mungu atafanya jambo na utabadilika barikiwa 🙏”, ameandika @anniemarie1118

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags