Zuckerberg ashinda medali mchezo wa karate

Zuckerberg ashinda medali mchezo wa karate

Mwanzilishi wa Facebook na ofisa mtendaji mkuu wa Meta, Mark Zuckerberg amewashangaza mashabiki na wapenzi wa mchezo wa karate baada ya kushinda medali za dhahabu na fedha katika mashindano yake ya kwanza ya jiu-jitsu  huko Brazil.

Pamoja na hayo bilionea huyo mwenye umri wa miaka 38, Mark Zuckerberg ameuthibitishia ulimwengu kuwa anao uwezo mkubwa hata nje ya teknolojia baada ya kuposti picha kwenye mitandao yake zinazomuonesha akishinda katika shindano lake la kwanza la BJJ na kuondoka na medali.

Pia mnamo mwaka 2022, Zuckerberg alimwambia Joe Rogan kuwa anavutiwa mno na michezo ya karate na tangu wakati huo amekuwa akifanya mazoezi.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags