Zuchu: Mimi na Diamond siyo wapenzi tena

Zuchu: Mimi na Diamond siyo wapenzi tena

Mwanamuziki wa Bongofleva nchini Zuchu ameweka wazi kuwa yeye na mpenzi wake ambaye pia ni Bosi wake Diamond kuwa hawapo kwenye mahusiano.

Zuchu kupitia ukurasa wake wa Instagram ame-share ujumbe huo uliokuwa ukieleza kuwa, imemuwia ugumu kulisema suala hilo lakini ameamua kuweka wazi kuwa yeye Diamond hawako pamoja huku sababu kubwa akieleza kuwa ni kukosa heshima kutoka kwa msanii huyo.

“I know this has been our thing but as hard as it is kumuacha mtu unaempenda hii naomba mungu iwe ya mwisho na nianze maisha mapya mapenzi ni heshima kwa bahati mbaya sana hiko kimekosekana kwetu.

As for him bado tuna kazi za pamoja i wish him and his family the absolute best, tumeishi vizuri lakini nadhani hii sio rizki mwaka huu nimejifunza kusema hapana kwa kila kitu kisichonipa furaha ama baada ya kusema haya naona kabisa naenda kuanza ukurasa mpya wenye maisha yaliyojaa furaha ,uhuru na Amani”


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post