Zuchu: japo kuwa namchuna kang’ang’ania

Zuchu: japo kuwa namchuna kang’ang’ania

Huwenda mwanamuziki @officialzuchu , anakaribia kutoa wimbo mpya, kutokana na kionjo cha maneno ambacho ame-share kama caption kwenye picha aliyo-post katika ukurasa wake wa #Instagram.

Imekuwa kawaida ya wasanii hasa kwa mwanadada huyo , kuandika maneno katika picha zake na kisha badae maneno hayo yanakutwa kwenye nyimbo anazotoa.

Nikukumbushe kwenye wimbo uitwao #Nani ambao kaimba  msanii huyo, aliwahi ku-post picha na kuisindikia kwa swali liulizalo “nani anaweza kulicheza sagarumba?” Lakini badae mstari huo ukasikika kwenye wimbo aliotoa.

Kwa mara nyingine tena zuchu ame-post picha na kuandika maneno yasomekayo

“Japo kua namchuna ,kang’ang’ana humohumo, honey wangu akinuna ,namkatia viuno😜”

Huku chini ya maneno hayo Malkia wa Mipasho Tanzania @officialkhadijakopa, ambaye ni mama mzazi wa #Zuchu, hakupita kimya akadondosha comment yake isemayo.

“twende twende honeyyyyyyyyy @officialzuchu”.  Jambo hilo limezidi kuonesha kuwa pengine kuna ujio mpya wa kazi kutoka kwa #Zuchu .






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags