Zingatia muonekano huu siku ya graduation yako

Zingatia muonekano huu siku ya graduation yako

Alooooh!!! Karibu sana mdau na mfuatiliaji wa page ya fashion wiki hii bwana nakusogeza rasmi kwenye msimu wa graduation katika shule na vyuo mbalimbali hapa nhini.

Kama unavyofahamu bwana msimu wa graduation katika shule na vyuo mbalimbali nchini umewadia, katika kipindi hiki huwa kuna pirika za hapa na pale kwa wahitimu katika kutaka kupata muonekano wa tofauti katika siku yao hiyo muhimu.

Ili kupata muonekano huo wa kipekee haswa kwa wahitimu wa vyuo vikuu wanapaswa kuzingatia mambo mbalimbali ikiwemo uvaaji wa nguo' classic' zinazoendana na tukio lenyewe, uvaaji wa viatu rasmi vitakavyokufanya kuwa huru pamoja na upakaji wa makeup ya wastani kwa wahitimu wa kike.

Akizungumza na jarida la  Mwananchi scoop mtaalamu wa masuala ya urembo Aisha Mtawa anaeleza kuwa mahafali ni moja kati ya siku muhimu sana kwa mwanafunzi katika maisha yake ya kielimu hivyo ni muhimu aonekane classic.

Alisema mahafali ni sherehe lakini ipo katika mfumo rasmi hivyo ni vyema kuvaa nguo rasmi lakini zilizo classic na zenye mitindo ambayo itakufanya kutoka kitofauti.

"Zile nguo zetu za kumeremeta za kwenye harusi na sendoff, kwenye sherehe za mahafali siyo mahala pake,"anasema.

Pia ameshauri kwa wahitimu wa kike kujiepusha na uvaaji wa nguo fupi na zenye kubana sana kwani zinaweza kuwafanya kushindwa kuwa huru kusheherekea.

"Ili kupata mavazi yatakayokupa muonekano mzuri ni vyema kufanya maandalizi mapema na kufanya utafiti ni wapi utapata nguo nzuri au mbunifu wa mavazi atakayeweza kukushonea nguo itakayokupa muonekano mzuri katika siku hiyo muhimu" anasema.

Kwa upande wa viatu Aisha alisema uvaaji wa viatu mara nyingi huendana na tukio linalofanyika katika eneo husika hivyo kwa kuwa shughuli hiyo ni rasmi hivyo inapendeza zaidi wahitimu wa kike na kiume kuvaa viatu vilivyo rasmi na vitakavyowafanya kuwa huru zaidi.

"Piga picha mwanaume kavaa suti nzuri then chini akavaa sendo au ndala hii itaharibu mvuto wake  kutokana na kutokuwa na muunganiko kati ya nguo na aina ya viatu alivyovaa,"alisema.

Vilevile aliwataka wahitimu wa kike kuacha tabia ya kuiga kuvaa viatu virefu sana ambavyo hawana uwezo wa kutembea navyo hali inayowapa changamoto katika kutembea.

Katika upande wa masuala ya makeup na nywele  kwa wahitimu wa kike mtaalamu mwingine wa masuala ya urembo Jackline George alisema ni vyema wahitimu hao kujiepusha na usukaji wa nywele au rasta zenye rangi rangi kwani linaweza kuleta tafsiri tofauti kwa kuwa tukio hilo ni rasmi.

"Tukio hilo ni rasmi hivyo usukaji wa nywele za rangirangi au unyoaji wa mitindo isiyokuwa rasmi inaweza kuleta tafsi isiyo nzuri kwa wageni waalikwa.

Kwa upande wa makeup kwa wahitimu wa kike Jackline alisema ni muhimu kwani inafanya muonekano wake kuvutia zaidi na ni vyema kupaka simple makeup ambayo inadumu kwa muda mrefu.

Eiwaaaaah bila shaka kwa dondoo hii nimekukuna haswaaa mwanachuo mwenzangu basi fuatilia kanuni hizo na taratibu ili kuepuka kuwa kituko bwana katika siku yako aadhwimu.

Kwa wale wote ambao wanahitimu mwaka huu jarida la Mwananchi scoop linawapa heko na kuwatakia kheri katika maisha ya mbeleni enjoy your day mtu this is fashion bwanaaaa!!!.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags