Zingatia mambo haya unapoandaa nguo za kazini

Zingatia mambo haya unapoandaa nguo za kazini

I hope mko pouwa watu wangu wa nguvu, leo katika segment ya Kazi tumekusogezea kitu ambacho kitakusaidia wewe unayehangaika kila ifikapo asubuhi wakati wa kwenda kazini kwa kujiuliza uvae nini.

Kabla haujawaza nguo ya kuvaa na utatokelezea vipi kazini, yapo mambo kadhaa ambayo yanaweza kukusaidia kukupa muonekano mzuri unapokwenda ofisini, wapo ambao huvaa simple na wengine wanapenda kutupia kila siku.
Bila kupoteza haya ndiyo mambo ya kuzingatia unapoandaa nguo ya kuvaa kazini.


 Kuvaa nguo inayokutosha na inayoendana na umbo lako
Kabla haujaanda nguo yako ya kazini basi unachotakiwa kukizingatia ni kuchagua nguo inayokutosha kuvaa nguo ambayo haikutoshi haileti muonekano mzuri. Vaa kitu kinachoendana na wewe ili uwe huru katika mazingira ya kazini, na hapa ni kwa pande zote mbili kwa wanawake na wanaume

 Chagua rangi zinazokupendeza
Kama tunavyojua sehemu ya kazi kuna macho ya watu wengi haswa ukikuta ofisi kubwa hivyo kabla hujaandaa nguo ya kesho kazini hakikisha unachagua rangi ambayo inakupendeza, katika fashion kila binadamu ana rangi tano ambazo ni lazima akivaa zimpendeze hivyo basi siyo lazima kila siku kuvaa rangi moja unaweza kubadilisha kila siku.

Kingine cha kuzingatia hapa ni kuepuka kuvaa kachumbali nafikiri nikizungumza hivi naeleweka, siyo tena umeambiwa rangi hizi zinakupendeza basi ndiyo uzichanganye zote kwa wakati mmoja, angalia rangi iliyopoa na uvae, pia epuka kuvaa nguo za kung’aa sana kazini.

 Pendelea kuvaa viatu official kazini
Hapa kwenye viatu tunaweza kuwazungumzia kina dada zaidi kwani wao ndiyo wafanyakazi namba moja ambao wanaharibu utaratibu wa uvaaji wa viatu kazini, sasa basi ukiwa unafikiria kesho uvae nguo gani na rangi ipi pia ufikirie ni kiatu gani kitakacho kupendeza ambacho pia hakitakupa usumbufu wa namna yoyote ile.

Kama tunavyojua kila kiatu na mahala pake pa kukivaa huwezi ukavaa highheels nchi 10 kazini huo utakuwa ni ushamba na dhambi ya fashion, ili usiweze kuharibu vazi lako kisa kiatu ulicho vaa pitia tovuti za mitindo na uangalie viatu ambavyo unaweza kuvitumia kazini.

 Epuka kuvaa Accessories nyingi
Sawa tunajua kuwa uvaapo accessorie inakuletea muonekano mzuri mbele za watu lakini wapo baadhi ya watu hawautendei haki urembo huo kwani baadhi yao hujaza kacha, saa pamoja na pete mbili au tatu kwenye mkono mmoja hii inaweza kukuharibia kabisa muonekano wako.

Hivyo basi kama wewe ni mpenzi wa saa basi kuwa hata na saa zako tano ambapo kila siku uamkapo kwenda kazini basi uwe na saa nyingine kuepuka kurudia rudia saa moja kila siku.

 Waombe watu wako wa karibu ushauri
Sawa tunajua wewe siyo mtu wa urembo sana lakini jitahidi sana unapoona umekwama huelewi uvae nini kesho basi omba watu wako wa karibu wakusaidie kuchangu nguo nzuri, na hapa unaweza kuomba msaada unapokuwa na kikao kazini au presentation yoyote.



Na kingine cha kuongezea ni mkoba, hii sasa ni kwa akina dada, ukishakuwa unafanya kazi basi kwenye kazi hakuna mtu mzima na hakuna mtoto wote saizi ya kati hivyo basi jitahidi kubadilisha mikoba pamoja na kutumia pochi za hadhi yako, achana na mikoba ya mtumba.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags