ZIJUE TABIA ZA MTU MKOSOAJI

ZIJUE TABIA ZA MTU MKOSOAJI

Leo tutaongelea tabia za watu wasumbufu duniani. Wanasaikolojia wamekuwa wakisoma tabia za watu tofauti na kugundua kuwa zinatofautiana kutoka na makuzi, malezi na mazingira aliyokulia mtu.

Katika dondoo za Saikolojia tutaangalia tabia ya mtu anayeitwa mkosoaji. Huyu ni aina ya watu ambao ndani ya hisia zao hawana kitu kinachoitwa jema.

Kila jambo kwao utakalofanya wewe yeye akitazama atatoa kasoro. Watu hawa bwana ukipendeza kosa, usipopendeza kosa yani hana jema kwa kila kitu ambacho kinafanyika katika jamii.

Kwa mwanaume au mwanamke kama ameolewa na mtu wenye tabia hii asitegemee kabisa kutiwa moyo, kusifiwa, kupongezwa hivyo vitu vitatu havipo kabisa kwa mtu mwenye tabia ya ukosoaji.

Tabia ukosoaji hii mtu anakuzwa nayo kutoka kwa wazazi wake au katika jumuiya anayoishi hata ukienda kulalamika katika familia aliyokulia watakukosoa kwa sababu wenyewe wamezoea hayo maisha.

Tabia za mkosoaji ni hizi

Mtu huyu siku zote hudumu katika kulalamika na kunung'unika kwa kila jambo atakalofanyiwa like nzuri au baya.

Mara zote hutoa ushauri usiotakiwa au utakaoleta malalamiko kwa wengine. Yeye mwenyewe hawezi kufanya kila njema bali hudumu katika kulalamika.

Mtu huyu hujitahidi sana kusikiliza na kutafuta makosa kuliko kushika njema.

Jinsi ya kuchukuliana na mtu mwenye tabia ya mkosoaji

Waonyeshe kwamba unajali kwa kuwasikiliza wape nafasi ya kuongea nawe ujitahidi kuwasikiliza.

Wape changamoto watoe masuluhisho sio kasoro peke yake wanapotoa kasoro upande moja upande mwingine wakupe suluhisho.

Watahadharishe watu wako kuhusu simu wanayoweza kueneza kwa kukosa na kulalamika.

Chukuliana naye kwa upendo.

Dawa ya mkosoaji

Kwa hiyo wewe mwenye roho ya kukosoa tuonyeshe la kwako dawa ya mkosoaji mwambie sawa type suluhisho mara zote mkosoaji hana suluhisho mkononi wana tabia ya kuona ubaya tu

Pia jitahidi kumfundisha kutokosea kwa kila jambo ingawa itachukua muda mrefu kuwa na mawazo chanya lakini itasaidia kubadilika vichache sio vyote.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags