Duniani kuna tuzo nyingi kwenye sekta ya muziki ambazo hutolewa kama ishara ya heshima na mafanikio katika tasnia hiyo. Kati ya vitu ambavyo wasanii huvihesabu kama sehemu ya mafanikio ni ushindi wa tuzo hizo. Hivyo basi zifahamu tuzo kubwa duniani na maana zake
Grammy Awards ni mojawapo ya tuzo za muziki maarufu zaidi ulimwenguni zinazotolewa kila mwaka na Chama cha Watengenezaji wa Rekodi za Amerika (Recording Academy) tangu mwaka 1959. Tuzo hizo zilianzishwa kwa lengo la kutambua ubora katika uandishi wa nyimbo, utendaji wa muziki na ubora wa sauti, zinatolewa kwa vipengele mbalimbali vya muziki kama vile albamu bora na nyinginezo.
Tanzania Music Awards (TMA) ni tuzo za muziki zinazotolewa kila mwaka nchini Tanzania. Awali zilifahamika kama Kilimanjaro Music Awards. Tuzo hizi zilianzishwa mwaka 1999 na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).
BRIT Awards ni tuzo za muziki za Uingereza ambazo zilianzishwa mwaka 1977 na British Phonographic Industry (BPI). Tuzo hizi zinatolewa kila mwaka kwa lengo la kutambua mafanikio ya wasanii wa muziki wa pop na rock nchini Uingereza.
MTV Video Music Awards (VMAs), ni tuzo za muziki zinazotolewa na Kituo cha Televisheni cha MTV tangu mwaka 1984. Tuzo hizi zinazingatia ubora wa video za muziki na huwapa wasanii heshima kwa kazi zao ya ubunifu katika video zao.
American Music Awards (AMAs) ni tuzo za muziki zinazotolewa kila mwaka nchini Marekani na American Broadcasting Company (ABC) tangu mwaka 1973. Tuzo hizi zinategemea kura za mashabiki kupitia mitandao na hutolewa kwa kuzingatia wasanii wa muziki wa aina mbalimbali.
Billboard Music Awards ni tuzo za muziki zinazotolewa na jarida la Billboard kwa kutambua mafanikio ya wasanii na albamu kwenye chati za Billboard. Tuzo hizi zilianzishwa mwaka 1990 na hutegemea takwimu za mauzo ya rekodi, kupigwa redioni na mauzo ya muziki mtandaoni.
The Grammy Lifetime Achievement Award, hii ni tuzo ya pekee inayotolewa na Recording Academy kwa kutambua mchango wa kipekee wa wasanii katika tasnia ya muziki kwa muda mrefu.
Rock and Roll Hall of Fame Induction, hii ingawa si tuzo ya moja kwa moja, Rock and Roll Hall of Fame ni heshima kubwa kwa wasanii wa muziki wa rock. Wasanii hupatiwa kama sehemu ya kutambua mchango wao wa kipekee katika muziki wa rock.
MOBO Awards, ni tuzo za muziki za Uingereza zinazotolewa kwa wasanii wa muziki wa Kiafrika na Caribbean na wale wanaotumia muziki wao kushawishi jamii katika masuala mbalimbali. Tuzo hizi zilianzishwa mwaka 1996 na zinatambua mafanikio ya wasanii katika aina mbalimbali za muziki, ikiwa ni pamoja na hip-hop, R&B, reggae na muziki wa dancehall.
Tuzo za Oscar au Academy Awards, zilianzishwa na Academy of Motion Picture Arts and Sciences (AMPAS) mwaka 1929. Tuzo hizi zilianzishwa kwa lengo la kutambua ubora wa kazi katika tasnia ya filamu duniani.
Leave a Reply