Zelensky akanusha kutaka kumshambulia Putin

Zelensky akanusha kutaka kumshambulia Putin

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amekanusha kuwa nchi yake haikufanya shambulio linalodaiwa kuwa ni la ndege isiyokuwa na rubani dhidi ya Kremlin, ambapo Urusi inasema lilikuwa ni jaribio dhidi ya maisha ya Vradimir Putin.

Ofisi ya rais wa Urusi ilisema kuwa vikosi vya ulinzi vya nchi hiyo vilizidungua ndege mbili zisizo na rubani usiku hali ambayo ilitishia kisasi .

Rais Volodymyr anasema “Hatumshambulii Putin wala Moscow  tunapigania kwenye eneo letu kwasababu ya kulinda vijiji vyetu na miji yetu” alisema Volodymyr akizungumza katika ziara nchini Finland.

Aidha picha za video ambazo hazijathibitishwa zinazozunguka kwenye mtandao zinaonyesha moshi ukipaa juu ya Kremlin eneo kubwa la makao makuu ya serikali lililopo katikati ya mji wa Moscow

Video ya pili inaonyesha mlipuko mdogo juu ya jengo la seneti, huku wanaume wawili wakionekana kupanda kwa shida juu kabisa ya jengo hilo la bunge.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags