Zari na tuhuma za kuvunja ndoa ya mpenzi wake Shakib

Zari na tuhuma za kuvunja ndoa ya mpenzi wake Shakib

Mwanadada anaetikisa Zaidi kupitia mitandao ya kijamii Zarinah Hassan maarufu kama  (Zarithebosslady) Yupo kwenye Shutuma Nzito za kusababisha ndoa ya mpenzi wake aliekuwa nae kwa kipindi hiki Shakib kuvunjika.

Siku chache zilizopita katika ukurasa wake wa Instagram aliweka picha akiwa na Mpenzi wake huyo walizopiga kwenye party yake iliofanyika kwao Uganda.

Basi bwana Moja ya Wafuasi wake katika Mtandao huo alimtaka kujibu tuhuma za Kuvunja Ndoa ya Mpenzi wake huyo ambapo Kuna mwanamke Tayari ameshatoa Malalamiko hayo.



Siku chache zilizopita, Mwanamke Mmoja kutoka Uganda ambae ni mkazi wa  Marekani aliyetambulika kwa jina la  Nalule Shamirah Sembatya maarufu kama (mimi) alimshutumu Zari kwa kumpokonya mume wake Shakib Lutaaya huku akiambatanisha na Vyeti vya Ndoa ambapo vinaonesha walifunga Ndoa Mwaka 2016, June na Kusema kuwa hakuwahi kupewa Talaka .

Mbali na hivyo mimi alisema kuwa Mwaka Mmoja baada ya Ndoa yao alimpambania mume wake huyo kupata Visa ya Marekani Lakini baada ya Muda Mume wake alitoweka Nyumbani na kuanzisha Mahusiano na mwanadada Zari ambae anadai amemfuata kwa sababu ya Mafanikio alionayo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags