Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Njombe, Dkt. Isaya Mwasubila, amesema tafiti zimebaini maambukizi makubwa ya ugonjwa wa usubi katika maeneo 4 ambayo ni Itipula 30%, Igola 11.22%, Mji Mwema 5.68% na Mamongolo 4%
Wizara ya afya imeanza kampeni ya kutoa dawa ili kuwakinga wananchi ambao hawajapata ugonjwa huo, na kutoa tiba kwa walioathirika.
Ugonjwa wa usubi husababishwa na minyoo inayotokana na nzi weusi kupitia vyanzo vya maji yaendayo kasi. Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2022, halmashauri 29 nchini zilikuwa na maambukizi, huku 7.02% ya watu wakiwa hatarini kuambukizwa.
Leave a Reply