Young Soo ahukumiwa kwenda jela miezi nane

Young Soo ahukumiwa kwenda jela miezi nane

Muigizaji maarufu kutoka nchini Korea Oh Young-soo, ambaye alijulikana zaidi kupitia filamu yake ya ‘Squid Game’ amekutwa na hatia kwenye kesi ya unyanyasaji wa kingono na utovu wa maadili, na kupelekea kuhukumia kifungo cha miezi nane jela.

Hukumu hiyo imetolewa leo Ijumaa Machi 15, katika Mahakama ya Wilaya ya Suwon nchini Korea Kusini ambapo pia aliamuriwa kuhudhuria masomo ya saa 40 ya unyanyasaji wa kingono pamoja na kutojihusisha na shughuli za uigizaji kwa miaka miwili.

Hukumu hiyo inakuja baada ya muigizaji mwenzake wa kike ambaye hakutajwa jina lake kufungua kesi ya kufanyiwa unyanyasaji wa kingono tukio ambalo linadaiwa kutokea mwaka 2017 wakati wa ku-shoot filamu.

Kufuatia hukumu hiyo inasababisha muigizaji huyo kuondolewa katika filamu ya ‘Squid Game msimu wa pili’ ambayo inatarajia kutoka mwaka huu, pamoja na kuondolewa kwenye filamu iitwayo ‘About Family’.

Licha ya kukutwa na hatia Oh Young-soo amekana shitaka hilo huku vyanzo vya karibu vya muigizaji huyo vikidai kuwa anampango wa kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo.

Oh Young-soo ameonekana katika filamu mbalimbali zikiwemo ‘The Return of Iljimae’, ‘God of War’, ‘Chocolate’ na nyinginezo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags