Yanga yamfukuzisha kazi kocha wa Medeama

Yanga yamfukuzisha kazi kocha wa Medeama

Baada ya kupokea kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Yanga kwenye mchezo wa hatua ya makundi wa Ligi ya Mabingwa Afrika, uliochezwa Desemba 20, Medeama ya Ghana imemfuta kazi kocha wake mkuu, Evans Adotey kutokana na matokeo hayo mabaya.

Evans amekiongoza kikosi cha medeama katika michezo minne ya hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika na kuvuna alama nne na kushika nafasi ya mwisho kwenye kundi D, linaloongozwa na Al Ahly ‘mechi’ tatu ‘pointi’ tano, nafasi ya pili Yanga mechi nne pointi tano na ya tatu ni CR Belouizdad mechi tatu pointi nne. 

Hata hivyo, baada ya kufutwa kazi kama ‘kocha’ mkuu, ‘timu’ hiyo imempa majukumu mengine ya ukurugenzi wa fundi wa klabu hiyo cheo ali-chokuwa nacho awali katika timu hiyo kabla ya kuwa kocha mkuu. 

Katika Ligi Kuu Ghana ‘kocha’ huyo amekiongoza kikosi hicho katika mechi 11, nakuvuna pointi 16, akishika nafasi ya 12 katika ‘timu’ 18 na ameshinda ‘mechi’ tano, amepoteza tano na sare moja.

Katika hatua ya makundi Medeama bado ina michezo miwili dhidi ya Al Ahly na CR Belouizdad






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags