Yajue matumzi ya simu kitaaluma

Yajue Matumzi Ya Simu Kitaaluma

Post Descriptions

Sehemu ya kwanza

Na Shabani Kaluse

Kwani wewe ni nani...?

Tuko kwenye dunia ya utandawazi na mawasiliano yamerahisishwa sana kiasi kwamba kila kitu kiko kwenye viganja vyako.

Kila kitu kina faida na hasara zake. Hivyo basi hata matumizi ya teknolojia ya mawasiliano nayo ina faida kubwa sana iwapo utaitumia kwa busara au hasara kubwa sana iwapo hutakuwa na busara na kutokuwa mwangalifu.

Kuna jambo moja ambalo limekuwa likinisumbua sana hususan kwa vijana wa leo.

Jambo lenyewe ni kuhusu matumizi ya simu.  Licha ya matumizi yao ya simu binafsi lakini hata wale waliojiriwa kwenye idara ya mapokezi bado unaweza kukuta hawajui namna nzuri ya kupokea simu na kumsaidia mteja.

Naomba nianze na matumizi ya simu binafsi.

Hapa kuna tatizo kubwa sana hususan kwa dada zetu. Wengi hawajui matumizi ya simu kitaaluma. Nasema kitaaluma nikimaanisha in proffesional.

Nikisema In proffesional namaanisha nini?

Ni utaratibu unaokutambulisha kwa watu wengine kwamba umeelimika na kustaarabika kitaaluma kwa kiasi gani. Kwamba una uwezo wa kuwasiliana na watu wa kaliba mbalimbali kwa namna inayokutambulisha kwamba wewe ni nani.

Iko hivi.

Mara baada ya kumalizia masomo yao vijana huingia kwenye harakati za kutafuta ajira.

Watafanya maandalizi ya kuandaa taarifa zao zinazoonyesha majina yao, anuani zao, namba zao za mawasiliano, historia ya taaluma walizo nazo na uzoefu wao pamoja na wadhamini. Kwa kifupi hii inaitwa CV.

CV hiyo itatumwa sehemu nyingi zenye fursa za ajira na pia kwa jamaa na marafiki. Lengo kuu ni kutafuta fursa za kupata ajira au kuunganishwa na watu mbalimbali ambao wanaweza kuwaunganisha na sehemu zenye fursa za ajira.

Njia rahisi kabisa ya watu wenye fursa za ajira katika kuwasiliana na watu waliotuma CV zao kwao ni simu za mkononi. Utaratibu ambao unarahisisha mambo mengi.

Sasa kizungumkuti hususan kwa dada zetu kiko hapa.

Jamani sizungumzi jambo ambalo nimesimuliwa bali nazungumzia jambo ambalo nina uzoefu nalo kwa sababu natamani watu wabadilike na waende na wakati.

Katika nafasi yangu kazini nakutana na watu wengi sana ambao baadhi wana jamaa zao wanaotafuta ajira na kutokana na kufahamiana wengi hunipa CV za jamaa zao ili ikitokea fursa mahali nilipo niwaunganishe au kama kuna mahali pengine Labda nimesikia kuna fursa niwajulishe.

Sasa basi inatokea kuna fursa mahali nilipo ambayo nadhani inaweza kumfaa mmoja wa watu ambao nimeunganishwa nao.

 

Hatua ya kwanza kabisa ni kumpigia simu mhusika. Na huyo anayepigiwa simu hana namba yangu na hanifahamu kabisa.

Lakini naamini hilo siyo tatizo kwani kuwa na simu kunamuunganisha mtu na ulimwengu wa nje bila kujali wale anaowafahamu na asiowafahamu.

Na mtu anapoweka mawasiliano yake ya simu kwenye taarifa zake zinazomtambulisha kwa maana ya CV na kisha kuzisambaza hii tayari imepanua wigo wake wa mawasiliano kwa hiyo Muda wowote anatarajia kupigiwa simu iwapo imepatikana fursa.

Sasa shida iko hapa.

Unampigia mtu kwa ajili ya kumuita kwenye usaili na kwa kuwa namba unayompigia haipo phone book yake anapokea na kisha kukaa kimya akisubiri mpigaji aongee.

Hilo ni kosa kubwa sana la Kwanza.

Kosa la pili baada ya mpigaji kusema.... Hallo na kujibiwa hallo kavu kavu, mpigaji kwa kutokuwa na uhakika kama amepiga namba sahihi anaweza kuuliza, Samahani, naongea na nani?

Hapo utashangazwa na jibu kutoka upande wa pili.

'Kwani wewe ni nani?'

Halafu anaweza kuendelea...

'Kwanza si ni wewe ndiyo umenipigia...? '

Mpigaji anaweza kujitambulisha na kuuliza kama anaongea na fulani.

Hapo tena atajibiwa...

 

'Ehe, Ulikuwa unasemaje?

Mpigaji kwa utulivu atajitambulisha kwamba unapiga kutoka kampuni fulani na kumuuliza kama aliwahi kutuma CV yake katika kampuni hiyo.

Kwanza ataanza kusema....

'Mimi!, CV!, ahaaaa,  ndiyo niliwahi kutuma kweli. '

Baada ya hapo sauti itabadikika na kuwa ya nidhamu ya hali ya juu na shikamoo mpigaji wa simu atapewa.

Kwa bahati nzuri kidogo huyo kajitahidi. Lakini kuna wengine ukiuliza Labda unaongea na nani kwa mfano, simu inakatwa,  Na ukipiga tena haipokelewi.

Hao ndiyo vijana wetu wanaotafuta ajira ambao hawajui namna bora ya kupokea simu in proffesional…..

……Itaendelea wiki ijayo

 


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post