Yajue makundi ya damu pamoja na tabia zake

Yajue makundi ya damu pamoja na tabia zake

Kundi lako la damu linaweza kukufanya uwe dhaifu au imara katika kukabiliana na magonjwa fulani. Ni vyema kujua kundi lako la damu sawa na ilivyo vyema kujua mambo mengine yanayochangia kuwa na afya njema. Kujua kundi lako la damu Kunaweza kukuza uwezo wako wa kufahamu hatari zinazokukabili kutokana na kundi la damu ulilonalo na kuepuka hatari hizo kwa kutumia mtindo wa maisha unaofaa. Hata hivyo, Kama vilivyo viungo vingine vya mwili, damu nayo ina changamoto ya kukumbana na maradhi mbalimbali, magonjwa yanayoathiri utendaji kazi wa damu yanaweza kugawanywa katika makundi kama vile ya kurithi, kuambukiza, mabadiliko ya kimwili na saratani tofauti. Damu ya binadamu imegawanyika katika makundi makuu manne ambayo ni A, B, AB, na O, binadamu yeyote lazima awe na moja wapo ya makundi hayo.

 

GROUP A

Ni kundi la damu ambalo hupokea damu kutoka kundi O na kundi A tu na huweza kuchangia damu kwa kundi A mwenzie na kundi AB.

 • Hawa ni vegetarians. Yaani hutumia mbogamboga hasa za kijani. Pia wanahitaji sana mananasi na zabibu kwa wingi.
 • Mara nyingi ni wale watu ambao hawaambiliki yaani wakiamua kitu wameamua mpaka wakitekeleze.
 • Pia ni watu ambao ni wabishi sana au wabishani na hawakubali kushindwa.
 • Watu wa kundi hili pia huwa wana changamoto ya kuwa na upungufu wa acid mwilini hivyo hushindwa kuiprocess protini tumboni hasa itokanayo na nyama nyekundu.
 • Ni watu ambao hushambuliwa sana na saratani za mishipa ya fahamu, utumbo, mifuko ya mayai, mfuko wa kizazi na mlango wa uzazi kwa wanawake, kibofu cha mkojo, figo, kongosho na saratani ya kinywa, tezi za mate na umio.
 • Wana hatari pia ya kupatwa na magonjwa ya moyo, wako hatarini pia kupata kiharusi na ugonjwa wa shinikizo la damu.
 • Vyakula wanavyotakiwa kula kwa wingi ni mbogamboga za majani na nyama nyeupe, nyama nyekundu sio nzuri sana kwa watu hawa.
 • Hawatakiwi kutumia mara kwa mara vyakula hivi :- nyama nyekundu, ngano, machungwa na maziwa.
 • Wakila ndizi, maembe na mapapai huwasababishia waamkapo asubuhi kutokwa na makamasi kwa wingi.
 • Watu wa kundi hili wanapenda sana wali na mara nyingi ndio chakula chao kikuu.
 • Hawatakiwi kugusa kabisa ngano na mahindi na endapo wakatumia vyakula hivi hasa kwa wanawake huwasababishia kupata hedhi mara mbili kwa mwezi.

 

 Tabia zao ni hizi hapa:

 • Ni watu Wa gharama sana hasa wadada au wanawake.
 • Huishiwa au wanakuwa na upungufu wa damu sana.
 • Ni wavivu.
 • Ni wakweli
 • Ni wasiri sana.
 • Wanapenda kujifichajificha, kama ni usiku hupenda kukaa gizani sana.
 • Ni waaminifu sana na hapa mara nyingi unawakuta maafisa utumishi kwani hufuata sheria.
 • Ni watu ambao pia wanaumwa mara kwa mara, kutokana na upungufu wa kinga mwilini.
 • Wanapenda kuwa wao wao. Ni watu ambao wanafanya maamuzi wakiwa pekee yao.
 • Sio wazurulaji (Anaweza jifungia ndani asubuhi mpaka jioni na ukadhani hamna mtu)
 • Wakipenda wanapenda kweli.
 • Wanahitaji uwajali sana tunapokuja kuongelea mahusiano.
 • Wanadeka mno.

 GROUP B

Ni kundi la damu ambalo hupokea damu kutoka kundi O na kundi B tu na huweza kuchangia damu kwa kundi B mwenzie na kundi AB.

 • Hili ni kundi la watu ambao ni wazungumzaji yaani ukiwapa nafasi ya kuzungumza ni kama vile umekosea na hapa mara nyingi unawapata watu kama MCs, wasanii, watangazaji wa redioni.
 • Ni watu ambao wana tabia zilizojitosheleza yaani wamekamilika.
 • Wanapenda kuonekana, hapa utawakuta waimbaji na wamekamilika
 • Ni watu ambao husumbuliwa sana au wako hatarini kupata magonjwa kama uvimbe wa fizi na pia wanawake walioko katika kundi hili wako hatarini kupata ugonjwa wa kisukari aina ya pili.
 • Mara nyingi ni watu ambao wakipata maambukizi ya virusi vya aina yoyote ile huwa machizi au vichaa kutokana na kwamba vinaenda kuharibu mfumo wake wa fahamu, wana uwezo mkubwa kukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu.
 • Wana hatari kubwa ya kupata saratani ya koo.
 • Watu wa kundi hili hawashauriwi sana kula vyakula vya aina ya kuku (Mara nyingi wao wenyewe tu hawapendi kuku ingawa hawaruhusiwi kula), karanga, korosho na nyanya, hizi pia hawashariwi kula.
 • Ni watu ambao wanaamini sana kupitia maamuzi yao binafsi.
 • Si rahisi kuingia katika mradi wowote labda, umempa ufafanuzi wa kutosha kuhusiana na huo mradi.
 • Ni watu wa malengo, yuko tayari kupambana kuhakikisha anapata matokeo.

 

 GROUP AB

Ni kundi ambalo hupokea damu kutoka makundi yote ya damu lakini huweza kuchangia damu kwa kundi AB tu.

 • Hawa ni watu ambao mara nyingi hawaeleweki yaani wana tabia za A na pia tabia za B wakati mwingine.
 • Kundi hili la damu husadikika ni kundi linalopenda sana dini. Na mara nyingi washehe, mapadre, wachungaji utakuta wengi wapo kundi hili.
 • Ni wakarimu sana na wanapenda sana watu.
 • Hujitolea kwa ajili ya wengine. Mtu wa jamii, huyu anaweza kukupa kila kitu akabaki hana kitu.
 • Ni watu ambao wanaweza akaanzisha kitu asikimalizie ukakuta kaishia katikati halafu kaanzisha kingine.
 • Ni watu ambao wako hatarini kupata magonjwa kama kiharusi, dengue, magonjwa ya moyo, shinikizo la moyo na lehemu kujaa kwenye mishipa ya damu.
 • Watu wa kundi hili mara nyingi wakifikia uzeeni, uwezo wao wa kufikiri hupungua kwa haraka. Lakini mara nyingi kupungua kwa uwezo wa kufikiri hutokana na magonjwa kama shinikizo la Moyo, kisukari na lehemu kuwa nyingi sana mwilini.
 • Ni watu ambao wana uwezo mkubwa sana wa kukabiliana na magonjwa, yaani kinga yao ya mwili ni imara ukifananisha na makundi mengine yote ya damu.
 • Ni watu ambao wako na hasira za ndani kwa ndani, sio rahisi kuexpose hasira zake ukamtambua kirahisi.
 • Hubadilika kulingana na mazingira (Hawana tofauti na vinyonga).
 • Wanasifa ya uongozi.

 
GROUP O

Ni kundi ambalo huweza kuchangia damu kwa makundi yote lakini hupokea damu kutoka kundi O tu.

 • Hawa ni watu ambao ni jeuri na kiburi na wanajiamini sana.
 • Wanasifa ya uongozi. Wanapenda kuongoza watu.
 • Wazurulaji mno.
 • Ni wawazi.
 • Watu ambao ni wababe, wagumu na wanafanya maamuzi yao pale wanapoamua na sio kulazimishwa.
 • Watu ambao hawapendi uongo.
 • Ni watu ambao wanaweza jihusisha na mahusiano zaidi ya moja na wakaona wako sawa.
 • Ni watu ambao sio rahisi sana kupata shambulio la ghafla la moyo kama ilivyo kwa watu wenye makundi mengine ya damu.
 • Hawana kinga ya kutosha dhidi ya kipindupindu lakini wana kiasi fulani cha kinga dhidi ya kifua kikuu (TB), malaria isiyo kali, saratani za kongosho, tumbo, matiti na mlango wa kizazi.
 • Ni rahisi kupata magonjwa ya maambukizi ya Ngozi na vidonda vya tumbo. Wanapata sana maumivu ya kiuno, magoti pamoja na mgongo.
 • Ni watu wasiopenda vitu vichachu kutokana na uwepo Wa acid kwa wingi mwilini mwao hivyo wanasumbuliwa sana na vidonda vya tumbo na huwa wanasumbuliwa sana na tatizo la choo (constipation) pamoja na kisukari.
 • Kundi hili pia hutokewa na mvi za mapema sana.
 • Kwa wanaume hapa ndipo unawakuta ambao wana mapaja yasiyolingana yaani moja kubwa, lingine dogo.
 • Wapunguze kula ngano na mahindi mara kwa mara.
 • Wapunguze kula machungwa, passion, ukwaju, maembe mabichi, zabibu nk.
 • Wanaume walioko katika kundi hili wanahitaji protein kwa wingi kuliko wanawake kutokana na kuhitaji nguvu kwa sana katika shughuli zao na miili yao kwa ujumla.
 • Kwa wanaume wanatakiwa kula matunda sana kama maembe, mananasi, ndizi, matikiti maji (ule na mbegu zake) hapa pia kama ni tunda unakula lote mfano nanasi unalimaliza, papai unalimaliza na pia matunda ya rangi moja kula kwa pamoja.
 • Vyakula vinavyowasaidia au wanavyohitaji sana mwilini ni matunda, mboga za majani, protein kwa wingi yaani nyama, maharage, mayai na maziwa.

TAFAKARI

Magonjwa mengi yanaweza kuepukwa kwa kuzingatia usafi wa mwili na mazingira, mlo kamili (kula kilingana na uhitaji wa group lako la damu), kufanya mazoezi, kupunguza uzito uliozidi na kuepuka matumizi ya tumbaku, pombe pamoja na madawa.

Imeandaliwa na Mark Lewis


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Detricia Pamba

A Digital Journalist, Content Creation Executive at Mwananchi Communications Ltd and Chief Editor of Mwananchi Scoop. I'm also writes stories around Technology, every Wednesday on Mwananchi Scoop. My other famous segments on Mwananchi Scoop include LISTI and WHO’S HOT.


Latest Post