WCW:MARIA BASSO

WCW:MARIA BASSO

Name: Maria Basso

University: University of dar es salaam

Position: Student

Course: Diploma of journalism

Year of study: Second year

Favorite sport: Wresting

Hobbies: Sing, writing, listening to Swahili podcasts

Dreams: Being a good person to others and help alot of people to be happy since it's easy to die and not easy to live at all.

MARIA BASSO: UMBILIKIMO NI KAMA GIZA UMENISAIDIA KUONA NYOTA

Kama kuna jambo nimejifunza mpaka hapa nilipo kwa walimwengu ni kujenga uhusiano wa kudumu na nafsi zetu,imani zetu na kuamini kila kitu kitakaa sawa japo huoni hata chembe ya muale wa mwanga kila ukipepesa macho.

Hili si gonjwa kwangu kwa sasa,kwani binadamu alie hai anakasoro wapo ambao zinaonekana na wale ambao zao zimekua Kama nyoka alie na miguu ya jongoo aliepotea miaka kenda,

Kuna machapisho niliyasoma kwamba mwanaume au mwanamke mfupi ana asilimia chache sana kupendwa kimapenzi wawili kati ya wanane huibuka kidedea na kuwa kwenye mahusiano.

Nilijihisi kama nina sifa za mkaa ama maiti maana sukuacha kulia na dunia nikiamini hakuna atakaekuja kuvutiwa na mimi kwa sababu ya umbilikimo wangu

Pasi na yote hayo nikajifunza kuwa "aliye kula kitovu chako hatukuacha utumbo" nilikua najidhulumu mwenyewe na kushindwa kujijua mimi ni nani na kuacha makelele ya wanadamu kuniambia mimi ni nani.

Ama kweli kuishi si rahisi sote tunajaribu ila ukiruhusu walimwengu wakuambie wewe ni nani basi utachelewa kuelewa msemo wa afae hakosi kuzikwa.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags