Waziri wa zamani Rwanda aswekwa jela miaka 5

Waziri wa zamani Rwanda aswekwa jela miaka 5

Mahakama kuu nchini Rwanda mjini Kigali imemuhukumu aliyekuwa waziri wa utamaduni nchini humo, kifungo cha miaka mitano jela kwa madai ya rushwa.

Rais Paul Kagame alimfukuza kazi Edouard Bamporiki mnamo mwezi Mei mwaka jana kabla ya waendesha mashtaka kutangaza kufanya uchunguzi juu yake kuhusu matumizi mabaya ya madaraka na kutaka rushwa kutoka kwa mfanyabiashara wa eneo hilo.

Bw Bamporiki alikiri mashtaka hayo kwenye Twitter na kumuomba rais amsamehe, lakini mnamo Septemba mahakama ya awali ilimhukumu kifungo cha miaka minne, ambapo alikata rufaa.

Akisoma uamuzi wa mahakama siku ya Jumatatu jioni, hakimu alisema, "haki inahitaji kutolewa ili kuonesha mfano", kwa afisa huyo ambaye amekuwa chini ya kizuizi cha nyumbani tangu afukuzwe kazi.

Bamporiki mwenye umri wa miaka 39, mshairi na mtayarishaji filamu ambaye alipanda vyeo haraka sana kupitia chama tawala, anakabiliwa na kesi ya nadra sana kwa maafisa wakuu kuhukumiwa kwa ufisadi nchini Rwanda.

Wakili wake, Evode Kayitana, aliiambia BBC kwamba wanaweza kukata rufaa "ikiwa tutaonyesha ukosefu wa haki katika kesi", akiongeza kuwa bado hawajaamua kufanya hilo.

Chanzo BBC






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags