Waziri apiga marufuku kuwakataza watoto kwenda likizo

Waziri apiga marufuku kuwakataza watoto kwenda likizo

Waziri wa elimu,sayansi na teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema amepokea malalamiko kwamba kuna Shule zinazuia wanafunzi kwenda likizo bila kushauriana na wazazi.

Huku wazazi wengine wakitakiwa kulipa ili kuwaweka wanafunzi shuleni ambapo amewataka viongozi wa shule kutambua kuwa ni haki ya mwanafunzi kwenda likizo.

Aidha Mkenda amesema “Kwa Shule za Serikali kuna mwongozo umetolewa na kamishna wa Elimu kuwa siku za kufunga na kufungua Shule, ni muhimu sana tukajifunza kuzingatia huo mwongozo ili wanafunzi wapate muda pia wa kupumzika, nahimiza wakuu wa Shule wote na wakurugenzi wazingatie utaratibu huo”alisema waziri huyo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags