Wawili wadakwa kwa tuhuma za mauaji kwenye Super Bowl

Wawili wadakwa kwa tuhuma za mauaji kwenye Super Bowl

Wanaume wawili kutoka Marekani wameshitakiwa kwa mauaji baada ya kufyatua risasi na kusababisha vurugu kwenye sherehe za ushindi wa ‘Super Bowl’ mwaka huu huko Kansas City nchini Marekani.

Wanaume hao waliyofahamika kwa majina ya Dominic Miller na Lyned wamesababisha kifo cha mwanamke mmoja huku watu wengine 22 wakijeruhiwa kwa risasi.

Kwa mujibu wa mwendesha mashtaka Jean Peters ameeleza kuwa watu hao wameshafikishwa mahakamani na wameshitakiwa kwa makosa mawili likiwemo la kufanya mauaji na matumizi haramu ya silaha.

‘Super Bowl’ ni mchezo aina ya kikapu ambapo fainali yake hufanyika kila mwaka katika Majimbo mbalimbali nchini Marekani ikiwa chini ya usimamizi wa ‘ligi’ ya Taifa ya Soka la NFL.

Kwa mwaka huu upande wa burudani za fainali ya ‘Super Bowl’ mwanamuziki #Usher alionesha uwezo wake baada ya kufanya makubwa katika show hiyo ambayo ilipelekea kuvunja rekodi kwa kupata watazamaji zaidi ya milioni 123 akiipiku ya mwanamuziki #Rihanna iliyopata watazamaiji zaidi milioni 121.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags