Watumbukia kwenye bwawa baada ya jukwaa la sarakasi kuvinjika

Watumbukia kwenye bwawa baada ya jukwaa la sarakasi kuvinjika

Sehemu maarufu ya kivutio nchini Ujerumani ambayo juu  imewekwa  jukwaa la michezo ya waruka sarakasi huku upande wa chini kuna bwawa la maji, imetokea ajali baada ya jukwaa hilo  kuanguka ghafla na kusababisha wanasarakasi kutumbukia ndani ya bwawa.

Kutokana na tukio la kukatika kwa jukwaa hilo la kurukia sarakasi  "high-diving" na kudondokea ndani ya maji, imepelekea watu kujeruhiwa ikiwemo wasanii watano wa sarakasi na wageni wawili.

Watu wanne walilazimika kulazwa hospitalini kutokana na majeraha yao. Huku uvunjikaji huo umesababisha uharibifu mkubwa wa miundo iliyozunguka eneo hilo.

Sababu kamili ya ajali hiyo bado haijafahamika, kwa sasa polisi wanaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha ajali hiyo






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags