Watu wawili wafariki kwa ajali Mbeya

Watu wawili wafariki kwa ajali Mbeya

Wakati taifa likiwa kwenye majozi ya kuwapotenza ndugu zetu kwenye ajali ya ndege iliyotokea novemba 6 mkoani Kagera bila kusahau ajali ya gari Kiteto taarifa nyingine ya  kusikitisha hii hapa.

Watu wawili (2) wamefariki Dunia na wengine watatu kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari matatu baada ya basi la abiria kampuni ya Mangare Express linalofanya safari zake kutokea Mbeya kwenda sumbawanga kuzigoga gari nyingine Mbili katika mteremko wa Iwambi Mbeya.

Akithibitisha kutokea Kwa ajali hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna msaidizi wa Polisi Benjamini Kuzaga amesema chanzo Cha ajali hiyo, ni mwendokasi wa gari ya Mangare Express na kugonga gari ndogo aina ya raumu na kusababisha vifo Vya watu wawili waliokua kwenye gari hiyo.

ACP Kuzaga amesema hali za majeruhi watatu waliokua kwenye hiyo ni mbaya na wamekimbizwa kwenye hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya kwaajili ya kupatiwa matibabu.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post