Watu 7 wauwawa katika shambulio, Somalia

Watu 7 wauwawa katika shambulio, Somalia

Takriban watu saba wameuwawa siku ya jana wakati magari mawili yaliyobeba mabomu kulipuka nje ya kambi ya mafunzo ya kijeshi katika mji wa Bardhere, kusini mwa Somalia.

Moja ya chombo cha habari kimeripoti kuwa mkuu wa wilaya ya Bardhere, Mohamed Wali Yusuf, alisema vikosi vya usalama vya mkoa, vilizuia mabomu na kujitoa mhanga.

“Tulikuwa tumepata vidokezo vya kiusalama kuhusu uwezekano wa mashambulizi, na hilo lilitusaidia kuzuia mashambulizi na kuzuia magari ya kujitoa muhanga kufikia eneo hilo” alisema Yusuf.

Aidha wanamgambo wenye itikadi kali wa Al-Shabab walidai kuhusika na shambulizi hilo wakilenga kambi hiyo kwa sababu maafisa wa nchi ya Ethiopia na Somalia walikuwa wakikutana huko.

Mnamo mwezi machi mwaka huu, shambulio kama hilo la bomu lililotegwa ndani ya gari, lililenga hoteli katika eneo hilo na kusababisha vifo vya wanajeshi kadhaa na wengine 10 kujeruhiwa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags