Watu 310 Wafariki Pakistan

Watu 310 Wafariki Pakistan

Moja kati ya taarifa kubwa tuliyonayo ni hii hapa ambapo Takribani watu 310 wamefariki dunia huku wengine 300 wamenusurika kifo kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha na kusababisha mafuriko nchini Pakistan.

Mamlaka ya Taifa ya Kusimamia Majanga (NDMA) imetangaza taarifa hiyo na kueleza kwamba wanawake na watoto 175 ni miongoni mwa wahanga wa janga hilo.

Aidha Mamlaka hiyo imefafanua kuwa watu 64 wamefariki dunia Mashariki mwa Mkoa wa Punjab, 62 wamefariki Kaskazini Magharibi mwa Mkoa wa Khyber Pakhtunkwa na zaidi ya watu 70 wapoteza maisha Kusini mwa Mkoa wa Sindh.

Sambamba na hayo, mamlaka hiyo imeongeza kuwa nyumba 8,979 na takribani madaraja 50 yameharibiwa kwa kusombwa na maji ya mafuriko hayo katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.

Hata hivyo Taarifa inaeleza kuwa Jeshi la wanamaji la Pakistan linaendelea na operesheni za kutoa misaada kwa waathirika wa mafuriko sambamba na kuwahamisha watu wanaoishi kwenye maeneo hatarishi zaidi.

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags