Watoto wamkutanisha Jennifer Lopez na Ben Affleck

Watoto wamkutanisha Jennifer Lopez na Ben Affleck

Baada ya kuwepo kwa tetesi za mwanamuziki #JenniferLopezi na mumewe #BenAffeck kutengana na kuuza nyumba yao waliyokuwa wakiishi, hatimaye wawili hao wamekutana tena katika mahafari ya mtoto wao.

Tovuti ya TMZ News imeeleza kuwa siku ya jana Jumatano Jennifer na Ben waliweka kando ratiba zao na kuhudhuria katika sherehe ya kuhitimu shule ya msingi ya mtoto wao aitwaye Samwel.

Wanandoa ambao mpaka sasa ndoa yao inaukakasi licha ya kujumuika katika sherehe hiyo bado walikuwa na mipaka kati yao hali ambayo imezidi kuwapa maswali watu baada ya kukataa kupiga picha ya pamoja.

Hata hivyo mwimbaji huyo mkongwe mwenye umri wa miaka 54 na mumewe mwenye umri wa miaka 51,  pamoja na kuonekana penzi lao limekwisha lakini huenda bado kuna mapenzi kati yao hii ni baada ya kuonekana wakiwa wamevalia pete za ndoa.

Ikumbukwe kuwa wawili hao walianza mahusiano mwaka 2002 na kutengana kwa mara ya kwanza mwaka 2004, lakini Julai mwaka 2021 walithibisha kurudiana hivyo mwaka 2022 waliweza kufunga ndoa na kubahatika kupata watoto watano.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags