Watengenezaji iPhone kujitosa katika magari

Watengenezaji iPhone kujitosa katika magari

Kampuni ya kutengeneza iPhone Foxconn inaweka dau kubwa kwenye magari yanayotumia umeme na kufikiri upya mahusiano kati ya Marekani na China.

Katika mahojiano maalum, mwenyekiti na bosi Young Liu aliiambia baadhi ya vyombo vya habari kuwa nini mustakabali wa kampuni hiyo ya Taiwan.

Alisema hata Foxconn inapohamisha baadhi ya maduka yake ya usambazaji kutoka China, magari ya umeme (EVs) ndiyo yatachochea ukuaji wake katika miongo ijayo.

Huku mvutano wa Marekani na China ukiendelea kuzorota, Liu alisema, Foxconn lazima ajiandae kwa hali mbaya zaidi iwapo itatokea.

“Tunatumai amani na utulivu vitakuwa jambo ambalo viongozi wa nchi hizi mbili watazingatia,” Liu mwenye umri wa miaka 67 alisema, katika ofisi zake Taipei, mji mkuu wa Taiwan.

Matukio hayo yanaweza kujumuisha majaribio ya Beijing kuizuia Taiwan, ambayo inadai kuwa sehemu ya Uchina, au mbaya zaidi, kuvamia kisiwa hicho kinachojitawala.

Liu alisema "mipango ya mwendelezo wa biashara" ilikuwa tayari inaendelea, na akadokeza kuwa baadhi ya njia za uzalishaji, hasa zile zinazohusishwa na "bidhaa za usalama wa taifa" tayari zinahamishwa kutoka China hadi Mexico na Vietnam.

Chanzo BBC

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post