Watendaji 7 wasimamishwa kazi uwanja wa mkapa

Watendaji 7 wasimamishwa kazi uwanja wa mkapa

Serikali imewasimamisha kazi watendaji 7 wanaofanya kazi uwanja wa taifa (Benjamin Mkapa stadium) ambapo walisimamishwa kazi kutokana na hitilafu ya umeme iliyojitokeza katika mchezo wa Yanga dhidi ya Rivers United jana April 30.

Salum Mtumbuka (Kaimu Meneja wa Uwanja), Manyori Juma Kapesa (Mhandisi wa Umeme) na Tuswege Nikupala (Afisa Tawala), Maafisa wengine waliosimamishwa ni Gordon Nsajigwa Mwangamilo, Gabriel Mwasele, Yanuaria Imboru na Dkt. Christina Luambano.

Aidha Milinde Mahona ameteuliwa kuwa Kaimu Meneja wa Uwanja kuanzia leo Mei Mosi, 2023 na imeagizwa mechi zichezwe Alasiri/Jioni kwa muda mpaka tatizo litakapo tatuliwa.

Serikali imeomba radhi na kusema hitilafu ya umeme imetokana na jenereta linalotumika uwanjani hapo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags