Watanzania wengine kulisaka tena taji AGT

Watanzania wengine kulisaka tena taji AGT

Ikiwa zimepita wiki kadhaa tangu waruka sarakasi maarufu kutoka nchini Tanzania Ramdhani Brothers kuondoka na taji la AGT Fantasy League mashindano ya kusaka vipaji yaliyofanyika nchini Marekani, sasa kundi jingine la waruka sarakasi wajulikanao kama Hakuna Matata Acrobats wameripotiwa kushiriki msimu wa 19 wa mashindano ya ‘America’s Got Talent’.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Hakuna Matata wame-share video wakiwa katika Auditions ya shindano hilo huku wakiwaomba watanzani kuwasapoti ili waweze kuendelea mbele.

Hakuna Matata wanaungana na Ramadhani Brothers kuwa watanzania pekee ambao wamefanikiwa kushiriki katika mashindano hayo ambayo hukusanyisha watu kutoka kwenye mataifa mbalimbali.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags