Wasudan 20,000 wakimbilia Chad

Wasudan 20,000 wakimbilia Chad

Umoja wa Mataifa (UN) umesema kuwa kati ya watu 10,000 na 20,000 wamekimbia mapigano makali Sudan na kutafuta usalama katika nchi jirani ya Chad.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) limesema limesikitishwa sana na kuongezeka kwa ghasia nchini Sudan na kusema wengi wa wanaowasili Chad ni wanawake na watoto.

"Mahitaji muhimu zaidi ni maji, chakula, malazi, huduma za afya, ulinzi wa watoto na kuzuia unyanyasaji wa kijinsia," taarifa ya shirika hilo iliongeza.

Aidha mipango miwili ya kusitisha mapigano imeshindwa na mkuu wa jeshi la Sudan ambaye ndiye kiini cha mzozo huo, aliiambia Al Jazeera siku ya Alhamisi kwamba haoni umuhimu wa kufanya mazungumzo na kundi la wanamgambo kuwa chaguo sahihi.

Ghasia hizo zimesababisha mateso makubwa kwa watu wa Sudan ambao wamekwama katika makazi yao na hivyo kushindwa kupata chakula cha kutosha na maji safi. mpaka sasa haijabainika jinsi mzozo huo wa siku saba leo utaisha vipi.

Chanzo BBC






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags