Washukiwa wa mauaji ya AKA wanyimwa dhamana

Washukiwa wa mauaji ya AKA wanyimwa dhamana

Baada ya washukiwa watano kati ya saba wanaohusishwa kuhusika na kifo cha ‘rapa’ Kiernan Forbes maarufu AKA kuomba dhamana mwezi uliyopita, na sasa dhamana hiyo imekataliwa na Jaji Vincent Hlatshwayo wa Mahakama ya Durban nchini Afrika Kusini.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari mbalimbali nchini humo vimeripoti kuwa Jaji huyo alikataa dhamana hizo kutokana na kesi iliyofunguliwa siku chache zilizopita ikiwataka washukiwa kujibu kesi inayowakabili hivyo basi Hlatshwayo ameeleza kuwa itakuwa ni uzembe kwa mahakama kutoa dhamana.

Hivyo basi Mahakama imetoa amri kwamba washukiwa hao waendeleee kusalia kizuizini mpaka pale watakapojibu mashitaka yanayo wakabili.

Aidha kwa mujibu wa Jaji Hlatshwayo ameweka wazi moja ya sababu za baadhi ya washukiwa hao kuomba dhamana noja wapo ikiwa ni kuhofia usalama wao wawapo gerezani huku wakidhani kuwa huenda wakauawawa watakapokuwa gerezani.

Ikumbukwe kuwa Febriari 28 mwaka huu washukiwa hao walikamatwa na kufikishwa Mahakamani ambapo walitambulika kwa majina Siyanda Myeza (21), Lindokuhle Ndimande (29), Lindani Ndimande (35), ambao ni mtu na kaka yake, Lindokuhle Thabani (30) na Mziwethemba Myeza (36).

Mwanamuziki na mfanyabiashara AKA aliuwawa pamoja na rafiki yake Tebello "Tibz" Motsoane kwa kupigwa risasi nje ya mgahawa huko Durban February 10, 2023.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags