Wasanii wa Bongo kwenye playlist ya Kamala Harris

Wasanii wa Bongo kwenye playlist ya Kamala Harris

Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris, ametoa Spotify playlist yake ya nyimbo 25 za Wasanii wa Afrika ambazo anazikubali, alizozipa jina la “Safari Zangu: Ghana, Tanzania na Zambia”, kama sehemu ya kukuza muziki na kuwapa hamasa zaidi wasanii wa Afrika wakati huu ambapo anafanya ziara katika nchi hizi tatu ndani ya wiki hii.

Mtandao maarufu wa Billboard umeitaja orodha hiyo ya wasanii wa Nchi hizi tatu na nyimbo zao ambazo wapenzi wa muziki duniani wanaweza kusikiliza kupitia Spotify na platform nyingine, lengo likiwa ni kukuza wasanii na mdundo wa kiafrika.

Wasanii wa Tanzania nao hawakuachwa nyuma na waliotajwa kwenye orodha hiyo ni pamoja na Harmonize na wimbo wake mpya ambao video yake imeachiwa rasmi leo ya Single Again,  Zuchu (Utaniua), Alikiba (Mahaba) Jay Melody (Sawa), Mbosso (Shetani), Jux & Marioo (Nice Kiss), Darassa (No Body) , Marioo & Abbah (Lonenly), Platform & Marioo (Fall).

Aidha makamu huyo tayari ametua Ghana tangu jana ambapo pamoja na mengine anayoyapa kipaumbele kwenye ziara yake ikiwemo maendeleo ya kiuchumi, mabadiliko ya tabia nchi, usalama wa chakula na ongezeko la idadi ya vijana.

Pia anatarajia kukutana na wasanii wa Kiafrika ikiwemo wale ambao wapo kwenye playlist yake ili kuongea nao na kuona namna bora ya kuufikisha muziki wao kwenye masoko makubwa ya muziki nchini Marekani.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags