Wananchi wa Ludewa mkoani Njombe wameiomba Serikali kuwajengea vilabu kwa ajili ya pombe za kienyeji kutokana na maeneo yao kukosa huduma hiyo huku Serikali ikipoteza mapato ambapo wameanzisha mgomo wa kunywa pombe hadi wajengewe vilabu hivyo.
Ombi hilo limetolewa na Wananchi wa Kijiji cha Ludewa Mjiji kwa Mbunge wa Jimbo la Ludewa Joseph Kamonga na kutishia mgomo wa kunywa pombe mpaka Serikali itakapowasaidia kupata kilabu cha pombe za kienyeji.
“Wenzetu wote vijijini huku wana kilabu cha kijiji sisi miaka yote hatupati tunaomba sana kusaidiwa”
Aidha Diwani wa kata ya Ludewa Monicka Mchilo amesema lengo la kujenga kilabu cha kijiji lipo kwa kuwa fedha zipo na Serikali inatambua huduma hiyo na kuwahakikishia Wananchi kuwa uongozi wa kijiji unakwenda kukaa ili kuzungumza juu ya kuanza ujenzi huku Mbunge wa Jimbo hilo akiwaomba viongozi kuhalakisha zoezi kwa kuwa imekuwa ni kero kwa Wananchi wa hali ya chini.
Leave a Reply