Baadhi ya Shule za Msingi kumekuwa na tabia ya kuwachangisha wanafunzi pesa kwaajili ya masomo, hali ambayo inawalazimu wanafunzi wasio na uwezo wa kuchangia kuto hudhuria darasani.
Wanafunzi wa Darasa la 7 katika Shule ya Msingi Chanika, Dar es Salaam wazuiwa kuingia darasani kwa kutochangia Tsh.500 kwa ajili ya masomo ya kila siku huku kila Jumamosi wakitakiwa kulipa Tsh. 1000
Licha ya hivi karibuni kamishna wa Elimu, Dkt. Lyabwene Mtahabwa, alisema michango ni makubaliano kati ya Shule na wazazi, hivyo ni hiyari kulipa.
Leave a Reply