Wanafunzi watatu UDOM wafariki ajali ya gari

Wanafunzi watatu UDOM wafariki ajali ya gari

Wanafunzi watatu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) wamefariki dunia na wengine watano wamejeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea jana jioni katika moja ya barabara zilizopo chuoni hapo.

 Ofisa Uhusiano wa chuo hicho, Beatrece Baltazar amesema ajali hiyo imetokea jana saa 2.00 usiku.

Amewataja waliofariki kuwa ni Hana Meshack, Zira Mpenda, Mpeli Mahenge.

Beatrece amewataja waliojeruhiwa kuwa ni Fortunata Kingazi, Fibi Julius, Sifa Shora, Enica William na mwingine aliyetajwa kwa jina moja la Furahina.

Amesema majeruhi wa ajali hiyo wamelazwa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa na hali zao zinaendelea vizuri.

Taarifa zinasema wanafunzi hao walikuwa wanatoka katika mahafali ya dini yaliyokuwa yakifanyika chuoni hapo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Detricia Pamba

A Digital Journalist, Content Creation Executive at Mwananchi Communications Ltd and Chief Editor of Mwananchi Scoop. I'm also writes stories around Technology, every Wednesday on Mwananchi Scoop. My other famous segments on Mwananchi Scoop include LISTI and WHO’S HOT.


Latest Post

Latest Tags