Wanafunzi 50 wafukuzwa chuo kwa udukuzi wa malipo ya ada.

Wanafunzi 50 wafukuzwa chuo kwa udukuzi wa malipo ya ada.

Chuo Kikuu mkoani Iringa (UoI) kimewafukuza wanafunzi zaidi ya 50 wa shahada ya teknolojia ya habari (IT) baada ya kudukua mfumo wa malipo ya ada ambapo ilionekana wamelipa, na kugoma kulipa ada hiyo hata walipogundulika wamefanya udanganyifu.

Makamu mkuu wa Chuo, Prof. Ndilirio Urio, amesema wanafunzi 256 walifanya udanganyifu wa malipo na Chuo kiliagiza matokeo ya wanafunzi wote yafutwe.

 “Seneti ya chuo hicho ilikaa mei 24,2023 wale ambao wamekubali kulipa ada, kukiri na kuomba msamaha tumewasamehe, wale wachache waliokaidi kulipa wamefukuzwa.”alisema mkuu wa chuo Ndilirio Urio.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post