Wanafunzi 14 wafutiwa matokeo kwa kuandika matusi

Wanafunzi 14 wafutiwa matokeo kwa kuandika matusi

Baraza la Mitihani limefuta matokeo yote ya Wanafunzi 14 walioandika matusi katika upimaji wa kitaifa wa kidato cha pili mwaka 2022.

Necta pia imefuta matokeo yote ya Wanafunzi 213 ambao waliobainika kufanya udanganyifu katika upimaji wa kitaifa wa darasa la nne 2022 na pia Wanafunzi 52 ambao wamebainika kufanya udanganyifu katika upimaji wa kitaifa wa kidato cha pili mwaka 2022.

“Matokeo hayo yamefutwa kwa mujibu wa kifungu cha 5 (2) (1) na 0) cha Sheria ya Baraza la Mitihani sura ya 107 kikisomwa pamoja na kifungu cha 30(2) (b) cha kanuni za mtihani mwaka 2016”






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags