Walioondoka kwa kukidhalilisha chama, watafute uungwana wakati wa kurudi

Walioondoka kwa kukidhalilisha chama, watafute uungwana wakati wa kurudi

Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema , Freeman Mbowe amesema chama chao ni cha Kidigitali, yeyote anaweza kujiunga au kutoka na pia hakuna urafiki wa kudumu au uadui wa kudumu kwenye siasa.

Akijibu hoja kama CHADEMA ipo tayari kumpokea aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Dkt. Willibrod Slaa, Mbowe amesema “Mtu aliyekuwa Kiongozi Mwandamizi kwenye chama kama Dkt. Slaa ujio wake hauwezi kuwa kama Mwanachama mwingine wa kawaida, lazima kuna njia zifuatwe."

Ameongeza “Bado hajatufikia, ametoa kauli kali dhidi yetu na wakati mwingine kutuunga mkono lakini hatuna geti la kuzuia Wanachama wapya. Tunatamani walioondoka kwa kashfa na kukidhalilisha chama wanapotaka kurejea watafute uungwana wa kuzungumza na Viongozi wenzao kujua kipi kilienda tofauti.”


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post