Waliombagua Vinicius wapigwa faini

Waliombagua Vinicius wapigwa faini

Watu saba raia wa nchini ya Ispania waliohusika katika mashambulizi tofauti ya kibaguzi dhidi ya Winga wa Real Madrid Vinicius Jr wameadhibiwa na tume ya taifa ya nchini humo dhidi ya ukatili, ubaguzi wa rangi, chuki dhidi ya wageni (Xenophobia) na kutovumiliana katika Michezo.

Kati yao watu wanne walitozwa faini ya Euro 60,000 na kufungiwa kuhudhuria kwenye viwanja vya michezo kwa miaka miwili baada ya kuning’iniza sanamu nyeusi iliyovalishwa jezi ya Vinicius namba 20 kwenye daraja moja nchini humo.

Pamoja na watu wengine watatu walitozwa faini na kufungiwa kuhudhuria viwanja vya michezo kwa mwaka mmoja baada ya kutoa ishara za kibaguzi kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa nchini Brazil wakati wa mechi ya La Liga.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags