Waliofariki Kenya kwa kufunga wengine walinyongwa

Waliofariki Kenya kwa kufunga wengine walinyongwa

Baadhi ya wahanga wa dhehebu tata linaloendesha shughuli zake katika msitu wa Shakahola katika Kaunti ya Kilifi nchini Kenya, waliuawa kwa kunyongwa, yameonyesha matokeo ya vipimo vya miili ya baadhi ya watu 110 iliyofukuliwa.

Zoezi la uchunguzi huo lililoongozwa na mchunguzi mkuu wa miili wa serikali Johansen Odour jana katika Hospitali ya Malindi ulionyesha kuwa watoto wawili walikufa baada ya kuzibwa pua na mdomo.

Maafisa wa uchunguzi wa miili jana waliweza kuchunguza miili ya watoto tisa na mwanamke mmoja. Watoto walikuwa na umri wa kuanzia mwaka mmoja na nusu hadi miaka kumi, kulingana Dkt Odour.

“Kwa ujumla walikuwa na muonekano wa njaa kali, Lakini miili miwili ya watoto ilikuwa na rangi ya bluu kwenye kucha za vidole vyao vya mikono hali iliyosababishwa inayofahamika kama asphyxiation. Hii inamaanisha kuwa walinyimwa hewa ya oksijeni wakati walipokufa na hii inaweza kuashiria kuwa huenda walinyongwa ,” Dkt Odour alisema wakati alipokuwa akitoa taarifa ya uchunguzi.

Aidha Dkt Odour alisema kuwa kazi ya uchunguzi wa miili ilikuwa na changamoto mwanzoni kwani ilibidi waweke machine za X-ray kwa ajili ya kukadiria umri wa marehemu.

Huku Mackenzie anatarajiwa kufikishwa mahakamani leo mjini Malindi pwani ya Kenya.

Chanzo BBC






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags