Serikali Korea Kusini imeonya na kuzuia matumizi ya vifaa vya kutolea mabaki ya chakula kwenye meno ‘toothpicks’ kutokana na baadhi ya watu kuvikaanga na kuvila.
Serikali nchini humo iligundua suala hilo baada ya kusambaa kwa video mitandaoni zikiwaonesha watu mbalimbali wakikaanga vijiti hivyo vya 'plastiki', huku walaji wakidai kuwa vinaongeza ladha kwenye chakula.
Hata hivyo Wizara ya chakula ya Korea Kusini imesisitiza kwamba usalama wa vijiti hivi vya meno kama chakula haujathibitishwa, bali vimethibitishwa kama bidhaa ya usafi umalizapo kula.
Wizara imewataka watu kujiepusha na matumizi ya ulaji wa vijiti hivi, ikisema kuwa usalama wao kwa matumizi haujathibitishwa.
Leave a Reply