Wakwe wamkataa Kanye West

Wakwe wamkataa Kanye West

‘Rapa’ kutoka nchini #Marekani, #KanyeWest anadaiwa kutengana na mkewe #BiancaCensori baada ya familia ya Bianca kuomba mrembo huyo aachane na Kanye kutokana na tabia zake.

Familia ya Bianca imekuwa ikilalamika jinsi Kanye anavyoishi na mrembo huyo ambapo baada ya kuolewa tu Bianca maisha yake yalibadilika muonekano na hata mavazi jambo ambalo familia yake hawakubaliani nalo.

Kwa mujibu wa Daily Mail inaeleza kuwa marafiki na familia ya Bianca kwa pamoja wamekuwa wakimlazimisha amuache Kanye na adai talaka kwani amekuwa akimpangia hadi vyakula vya kula.

Kanye mwenye umri wa miaka 46 alimuoa Bianca Disemba 2022, mwezi mmoja tu baada ya taratibu za talaka ya Kanye na aliyekuwa mkewe Kim Kardashian kukamilika.
.
.
.
#MwanchiScoop
#BurudikaNasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post