Wakikutana Diamond na Doffi ni kivumbi tu

Wakikutana Diamond na Doffi ni kivumbi tu

Katika tasnia yoyote ni vyema kuwa na kitu kiitwacho ‘kemistri’ kwa watu wanaofanya jambo pamoja, mfano mzuri siku za hivi karibuni msanii Jux ameonekana kuwa na ‘kemistri’ nzuri na baadhi ya wasanii ikiwemo kwa G Nako na Diamond kwani ngoma alizo washirikisha wakali hao zimeonekana kwenda mjini kwa kiasi kikubwa.

Lakini pia upande mwingine sauti ya Diamond huwa ikikaa pamoja  na ya Koffi Olomide kutoka nchini Congo watu huonekana kuvutiwa na mchanganyiko wa sauti zao. Inawezekana ni ukubwa wa kila mmoja kati yao kukubalika kwenye nchi anayotoka, lakini ubunifu waliyonao unachangia ngoma zao kutembea.

Kwanzia kwenye ubunifu wa mavazi Koffi kama kawaida yake huwa anawavutia na kuwashangaza wengi aina ya nguo anazovaa na akiwa pamoja na Diamond basi lazima amvalishe pia nguo za aina hiyo.

Mzigo alioachia Diamond na Koffi masaa mawili yaliyopita unawaonesha wakali hao wakiwa kwenye pigo za aina yake huku jina la wimbo kama kawaida huwa halitoi maana kamili kama ilivyokuwa kwa wimbo wao wa mwanzo #Waah walioachia miaka miwili iliyopita na hadi sasa umefikisha watazamaji 141M kwenye mtandao wa YouTube, huu wa sasa unaenda na jina la aina yake unaitwa Achii.

 

Unapenda nini kutoka kwa Diamond na Koffi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags