Wake wawili wa Mr Ibu wafunguka

Wake wawili wa Mr Ibu wafunguka

Wake wawili wa marehemu mwigizaji Mr Ibu, Ifeyinwa Okafor na Stella-Maris Okafor wamehudhuria msibani kwa mume wao licha ya kutokuwa na maelewano mazuri kwa muda mrefu.

Kwa mujibu wa tovuti ya Bbc wanawake hao walifunguka mapito waliyoyapitia na Mr Ibu ambapo Ifeyinwa Okafor alisema kuwa aliolewa na Mr Ibu na kupata mtoto wa kwanza mwaka 1994 na kutengana mwaka 1997 alipojifungua mtoto wa kiume aitwaye Onyebuchi Daniel.

Aidha aliweka wazi alikuwa hayupo sawa na mwigizaji huyo lakini baada ya kusumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu alimpigia simu na kumuomba msamaha.

Huku mke wa tatu Stella-Maris Okafor, akidai kuwa toka mumewe afariki hana furaha na watoto wake watatu kutokana na matukio wanayoyafanya watoto hao baada ya baba yao kufariki.

Utakumbuka kuwa wakati wa sakata la Mr Ibu kuomba msaada kwa jamii wa kuchangiwa fedha kwa ajili ya matibabu baadhi ya watoto wake walidakwa na polisi kwa tuhuma za kuiba fedha za matibabu ya baba yao.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags