Wajue watoto wa nne aliowaacha Malkia Elizabeth II

Wajue watoto wa nne aliowaacha Malkia Elizabeth II

Elizabeth Alexandria Mary maarufu kama Malkia Elizabeth II alifariki dunia jana mchana, Septemba 8, 2022.

Malkia huyo ambaye alisherehekea Jubilee ya Silva mwezi Juni mwaka huu alikuwa ni mtu pekee kutokea familia ya kifalme aliyeweza kutimiza miaka 70 ya uongozi toka enzi.

Malkia Elizabeth aliutwaa Umalkia akiwa na miaka 25 tu baada ya kifo cha baba yake King George VI, mwaka 1952.

Alifanikiwa kuolewa na Marehemu Prince Philip, Duke of Edinburgh ambao kwa pamoja walifanikiwa kupata watoto wanne, ikiwemo mtoto wao wa kwanza King Charles III ambae ametwaa jina hilo tokea jana baada ya kifo cha mama yake.

Katika makala hii, wajue watoto hao wanne aliowaacha Malkia Elizabeth II:


KING CHARLES III

Huyu ndiye mtoto wa kwanza wa Malkia Elizabeth II na mumewe Prince Philip, ambaye kwa sasa ndie aliyerithi kiti cha ufalme. Charles Philip Arthur George alizaliwa Novemba 14, 1948 huko London. Kabla ya kutunukiwa ufalme, Charles III alijulikana kama Prince Charles, Prince of Wales, cheo ambavho anatarajiwa kurithi mwanae wa kwanza. Charles III aliwahi kumuoa Princess Diana, story ambayo ilibughubikwa na visa vingi sana mpaka kuachana kwao, hadi kifo cha Princess Diana ambae alifanikiwa kupata nae watoto wawili, William na Harry. Baadae Mfalme Charles alimuoa Camilla Parker Bowles ambae kwasasa anajulikana kama Queen Consort Camilla.


ANNE, PRINCESS ROYAL

Despite ya kwamba wengi humjua King Charles III zaidi, Malkia alibarikiwa watoto wengine watatu. Anne Elizabeth Alice Louise alizaliwa Agosti 15, 1950 akiwa ni mtoto wa pili na mtoto wa kike pekee wa Malkia. Anne, Princess Royal anakuwa mtu wa 16 katika mstari wa kurithi ufalme kutokana na mifumo iliyoundwa nchini Uingereza. Alitwaa title ya Princess Royal mwaka 1987. Aliolewa na Captain Mark Phillips ambaye pamoja wana watoto wawili - Peter Phillips na Zara Tindall, ila baadae aliachana nae na aliolewa tena na mumewe wa sasa Timothee Laurence.


PRINCE ANDREW, DUKE OF YORK

Mtoto wa tatu wa Malkia ni Andrew Albert Christian Edward, 'Prince Andrew,' aliyezaliwa Februari 19, 1960. Yeye anakuwa wa 8 katika mstari wa kurithi ufalme wa Uingereza. Pamoja na kuwa mtoto wa Malkia, Prince Andrew alighububikwa na skendo kadhaa ikiwemo unyanyasaji wa kingono kwa watoto, uliopelekea kujivua vyeo vyake ili kupisha upelelezi wa kesi yake inayoendelea. Alimuoa Sarah Ferguson mwaka 1986 na kwa pamoja wana watoto wawili - Princess Beatrice na Princess Eugene. Wawili hao waliachana mwaka 1996.




PRINCE EDWARD, EARL OF WESSEX

Huyu ndie mtoto wa mwisho wa Malkia. Alizaliwa kama Edward Antony Richard Louis, Machi 10, 1964. Yeye ni mtu wa 13 katika mstari wa urithi wa Ufalme. 

Prince Edward alitwaa tiyle ya 'Earl of Wessex' baada ya kumuoa Sophie Rhys-Jones mwaka 1999. Wawili hao wana watoto wawili - Lady Louise Windsor na James Viscount Severn.







Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Detricia Pamba

A Digital Journalist, Content Creation Executive at Mwananchi Communications Ltd and Chief Editor of Mwananchi Scoop. I'm also writes stories around Technology, every Wednesday on Mwananchi Scoop. My other famous segments on Mwananchi Scoop include LISTI and WHO’S HOT.


Latest Post

Latest Tags